Nenda

Macvoice

Compositor: Não Disponível

N-Next Level Music
Hmm mmh, ohhh
(Ayolizer)

Mmmh, siri ya mwezi
Siri ya nyota, siri ya angani
Siri ya njozi, usingizi
Siri ya kitandani
Ila siri ya penzi, siri ya moyo
Siri ya nani?
Siri ya chozi, ni maumivu, ndani kwa ndani
Mapenzi niliyaanzisha yakanifurahisha
Yakanibadilisha jamani
Na sio tu kumridhisha
Nikamthaminisha, nikamtambulisha nyumbani
Hasa leo yamekwisha yananidhalilisha
Yananiaibisha hadharani
Ila yote ni maisha, japo nahuzunika
Wakuninyamazisha ni nani?

Sijuti kukufahamu, ila najuta kukuamini
Kasuku ndege wangu, leo umekuwa bundi
Pokea zangu salamu, bado sijui nitapona lini
Umevunja moyo yangu, we ndo ulikuwa gundi

Ile siku unafungasha mabegi
Ulidondosha picha yako njonjo
Ndo ninayojilazia kwa bedi
Haki ya Mungu umenipiga zongo
Naomba msalimie shemeji
Haki ya nani amepata chombo
Na kama ukiskia nimededi
Jua ni mawazo msongo

Nenda, salama nenda
Nenda, salama nenda
Nenda, salama nenda
Nenda, salama nenda

Nikiwa na marafiki, kwenye sura naogopa
Ila moyo unasota
Nikiwa peke yangu siwezi
Chozi linanidondoka
Nahisi kama naota
Hivi kweli umeondoka?
Yanautesa moyo mapenzi
Mpaka kupenda naogopa
Umesema, hutaki tena kuiona sura yangu
Kwenye simu umefuta namba zangu
Ila jibu lipo kwa Mola wangu
Mi nasubiri
Kila baya, unasema ukitaja jina langu
Umesahau yote mazuri yangu
Basi nilindie madhaifu yangu
Unisitiri, maana

Sijuti kukufahamu, ila najuta kukuamini
Kasuku ndege wangu, leo umekuwa bundi
Pokea zangu salamu, bado sijui nitapona lini
Umevunja moyo yangu, we ndo ulikuwa gundi

Ile siku unafungasha mabegi
Ulidondosha picha yako njonjo
Ndo ninayojilazia kwa bedi
Haki ya Mungu umenipiga zongo
Naomba msalimie shemeji
Haki ya nani amepata chombo
Na kama ukiskia nimededi
Jua ni mawazo msongo

Nenda, (hey) salama nenda (Nenda salama, aaah)
Nenda, salama nenda (oooh, oooh)
Nenda, (ouuuh, oooh) salama nenda (Nenda salama, aaah)
Nenda, salama nenda
(Nenda salama, mmh oooh)
Mwenzako naogopa, -ogopa eehh, iyeaaaaah
Mmh oooh

Kila baya, unasema ukitaja jina langu
Umesahau yote mazuri yangu
Basi nilindie madhaifu yangu
Unisitiri

(Ka mix Lizer)

©2003- 2025 lyrics.com.br · Aviso Legal · Política de Privacidade · Fale Conosco desenvolvido por Studio Sol Comunicação Digital